Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 45 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿ٱتۡلُ مَآ أُوحِيَ إِلَيۡكَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَۖ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ تَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِۗ وَلَذِكۡرُ ٱللَّهِ أَكۡبَرُۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تَصۡنَعُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 45]
﴿اتل ما أوحي إليك من الكتاب وأقم الصلاة إن الصلاة تنهى عن﴾ [العَنكبُوت: 45]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Isome hii Qur’ani iliyoteremshwa kwako, na uifuate kivitendo, na utekeleze Swala kwa mipaka yake, kwani utunzaji wa Swala unamkataza mtu kuingia kwenye vitendo vya uasi na makatazo. Hivyo ni kwamba mwenye kuzitimiza nguzo zake na masharti yake, moyo wake unang’ara, Imani yake inazidi, hima yake ya kufanya mema inapata nguvu na matamanio yake ya kufanya mabaya yanapungua au yanaondoka. Na kwa hakika, kumtaja Mwenyezi Mungu katika Swala na isiyokuwa Swala ni jambo kubwa na bora kuliko kitu chochote. Na Mwenyezi Mungu Anayajua mnayoyatenda ya uzuri na ubaya, hivyo basi Atawalipa kwa hayo malipo makamilifu zaidi na yanayotosha zaidi |