Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 47 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿وَكَذَٰلِكَ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَۚ فَٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۖ وَمِنۡ هَٰٓؤُلَآءِ مَن يُؤۡمِنُ بِهِۦۚ وَمَا يَجۡحَدُ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَّا ٱلۡكَٰفِرُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 47]
﴿وكذلك أنـزلنا إليك الكتاب فالذين آتيناهم الكتاب يؤمنون به ومن هؤلاء من﴾ [العَنكبُوت: 47]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kama tulivyowateremshia Kitabu, ewe Mtume, wale Mitume waliokuwa kabla yako, vilevile tumekuteremshia Kitabu hiki chenye kusadikisha Vitabu vilivyotangulia. Basi wale tuliyowapa Kitabu miongoni mwa Wana wa Isrāīl wakamjua vile inavyotakikana wamjue, wanaiamini Qur’ani. Na kati ya hawa Warabu wa Kikureshi kuna wanaomuamini. Na hawaikanushi Qur’ani au kuzifanyia shaka dalili zake na hoja zake zenye ushahidi uliyo wazi isipokuwa makafiri ambao mienendo yao ni kukataa na kufanya ushindani |