Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 52 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿قُلۡ كَفَىٰ بِٱللَّهِ بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡ شَهِيدٗاۖ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱلۡبَٰطِلِ وَكَفَرُواْ بِٱللَّهِ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 52]
﴿قل كفى بالله بيني وبينكم شهيدا يعلم ما في السموات والأرض والذين﴾ [العَنكبُوت: 52]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, «Inatosha kuwa Mwenyezi Mungu ni Shahidi baina yangu mimi na nyinyi juu ya ukweli wangu wa kuwa mimi ni Mtume Wake, na juu ya kunikanusha kwenu mimi na kuirudisha kwenu haki niliyokuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Anavijuwa vilivyomo mbinguni na ardhini», hakuna kinachofichamana na Yeye chochote kile kilichoko ndani ya hivyo viwili. Na wale waliouamini urongo na wakamkanusha Mwenyezi Mungu, pamoja na kuwepo dalili hizi zilizo wazi, hao ndiyo wenye hasara ulimwenguni na Akhera |