Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 53 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿وَيَسۡتَعۡجِلُونَكَ بِٱلۡعَذَابِ وَلَوۡلَآ أَجَلٞ مُّسَمّٗى لَّجَآءَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ وَلَيَأۡتِيَنَّهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 53]
﴿ويستعجلونك بالعذاب ولولا أجل مسمى لجاءهم العذاب وليأتينهم بغتة وهم لا يشعرون﴾ [العَنكبُوت: 53]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wanakuharakisha, ewe Mtume, hawa washirikina wa watu wako uwaletee adhabu kwa kukufanyia shere. Na lau si Mwenyezi Mungu kuwa Amewawekea wakati wa kuadhibiwa wao duniani usiotangulia wala kuchelewa, ingaliwajia wao adhabu pale walipoitaka. Na kwa hakika itawajia ghafula na hali wao hawaitambui wala kuihisi |