Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 65 - العَنكبُوت - Page - Juz 21
﴿فَإِذَا رَكِبُواْ فِي ٱلۡفُلۡكِ دَعَوُاْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ فَلَمَّا نَجَّىٰهُمۡ إِلَى ٱلۡبَرِّ إِذَا هُمۡ يُشۡرِكُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 65]
﴿فإذا ركبوا في الفلك دعوا الله مخلصين له الدين فلما نجاهم إلى﴾ [العَنكبُوت: 65]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wanapopanda makafiri kwenye majahazi baharini, na wakaogopa kuzama, wanampwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia dua wakati wa shida yao. Na Anapowaokoa akawafikisha kwenye nchi kavu, na shida ikawaondokea, wanarudi kwenye ushirikina wao. Hakika yao wao, kwa kufanya hivi, wanagongana, wanampwekesha Mwenyezi Mungu kipindi cha shida na wanamshirikisha kipindi cha raha |