Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 103 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿وَٱعۡتَصِمُواْ بِحَبۡلِ ٱللَّهِ جَمِيعٗا وَلَا تَفَرَّقُواْۚ وَٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ كُنتُمۡ أَعۡدَآءٗ فَأَلَّفَ بَيۡنَ قُلُوبِكُمۡ فَأَصۡبَحۡتُم بِنِعۡمَتِهِۦٓ إِخۡوَٰنٗا وَكُنتُمۡ عَلَىٰ شَفَا حُفۡرَةٖ مِّنَ ٱلنَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنۡهَاۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ ﴾
[آل عِمران: 103]
﴿واعتصموا بحبل الله جميعا ولا تفرقوا واذكروا نعمة الله عليكم إذ كنتم﴾ [آل عِمران: 103]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Shikamaneni nyote na Kitabu cha Mola wenu na uongofu wa Mtume wenu, wala msitende ambayo yatapelekea kutengana kwenu. Na ikumbukeni neema kubwa ambayo Mwenyezi Mungu Amewaneemesha nayo, pindi mlipokuwa, enyi Waumini, kabla ya Uislamu ni maadui, Mwenyezi Mungu Akazikusanya nyoyo zenu juu ya kumpenda Yeye na kumpenda Mtume Wake, na akatia ndani ya nyoyo zenu mahaba ya kupendana wenyewe kwa wenyewe, hapo mkawa, kwa fadhila Zake, ni ndugu mpedanao. Na mlikuwa kwenye ukingo wa moto wa Jahanamu, Mwenyezi Mungu Akawaongoza kwa Uislamu na Akawaokoa na Moto. Na kama Mwenyezi Mungu Alivyowafunulia wazi alama za imani iliyo sahihi, hivyo hivyo Anawabainishia yote yale ambayo ndani yake muna kutengenea kwenu, mpate kuongoka kweye njia ya uongofu na mpate kuiandama ili msipotee mkaiepuka |