Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 102 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِۦ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسۡلِمُونَ ﴾
[آل عِمران: 102]
﴿ياأيها الذين آمنوا اتقوا الله حق تقاته ولا تموتن إلا وأنتم مسلمون﴾ [آل عِمران: 102]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi ambao mumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake, muogopeni Mwenyezi Mungu kwa namna inavyopasa mumuogope. Nako ni Atiiwe wala Asiasiwe, Ashukuriwe wala asikufuriwe na Akumbukwe wala Asisahauliwe. Na dumuni katika kushikamana na Uislamu wenu mpaka mwisho wa uhai wenu, ili mkutane na Mwenyezi Mungu na nyinyi muko katika hali hiyo |