×

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema 3:110 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:110) ayat 110 in Swahili

3:110 Surah al-‘Imran ayat 110 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 110 - آل عِمران - Page - Juz 4

﴿كُنتُمۡ خَيۡرَ أُمَّةٍ أُخۡرِجَتۡ لِلنَّاسِ تَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَتَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَتُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِۗ وَلَوۡ ءَامَنَ أَهۡلُ ٱلۡكِتَٰبِ لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۚ مِّنۡهُمُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَأَكۡثَرُهُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ ﴾
[آل عِمران: 110]

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: كنتم خير أمة أخرجت للناس تأمرون بالمعروف وتنهون عن المنكر وتؤمنون بالله, باللغة السواحيلية

﴿كنتم خير أمة أخرجت للناس تأمرون بالمعروف وتنهون عن المنكر وتؤمنون بالله﴾ [آل عِمران: 110]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Nyinyi, enyi uma wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni bora wa ummah na ni watu wenye manufaa zaidi kwa watu, mnaamrisha mema, nayo ni yale yanayofahamika uzuri wake kisheria na kiakili, na mnakataza maovu , nayo ni yale yanayoeleweka ubaya wake kisheria na kiakili, na mnamuamini Mwenyezi Mungu kikweli-kweli imani inayotiliwa nguvu na vitendo. Na lau kama Mayahudi na Wanaswara waliopewa Vitabu wangalimuamini Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na yale aliyowajia nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kama mlivyoamini nyinyi, lingekuwa hilo ni bora kwao dunianina Akhera. Katiika hao wako Waumini waukubalio ujumbe wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wanaoufuata kivitendo ujumbe huo, nao ni wachache. Na wengi wao ni watokaji nje ya dini ya Mwenyezi Mungu na twaa Yake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek