Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 120 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿إِن تَمۡسَسۡكُمۡ حَسَنَةٞ تَسُؤۡهُمۡ وَإِن تُصِبۡكُمۡ سَيِّئَةٞ يَفۡرَحُواْ بِهَاۖ وَإِن تَصۡبِرُواْ وَتَتَّقُواْ لَا يَضُرُّكُمۡ كَيۡدُهُمۡ شَيۡـًٔاۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا يَعۡمَلُونَ مُحِيطٞ ﴾
[آل عِمران: 120]
﴿إن تمسسكم حسنة تسؤهم وإن تصبكم سيئة يفرحوا بها وإن تصبروا وتتقوا﴾ [آل عِمران: 120]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa uadui wa watu hawa ni kwamba nyinyi, enyi Waumini, mpatwapo na jambo jema la ushindi au ngawira, wao hupatwa na butwaa na huzuni; iwapo mtapatwa na maudhi ya kushindwa au upungufu wa mali, watu na matunda, wao hulifurahia hilo. Na mkiwa na subira juu ya yaliyowafika na mkamuogopa Mwenyezi Mungu katika yale Aliyowaamrisha na Akawakataza nayo, hautawadhuru udhia wa vitimbi vyao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyazunguka yote wanayoyafanya hao makafiri ya uharibifu na Atawalipa kwayo |