Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 128 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿لَيۡسَ لَكَ مِنَ ٱلۡأَمۡرِ شَيۡءٌ أَوۡ يَتُوبَ عَلَيۡهِمۡ أَوۡ يُعَذِّبَهُمۡ فَإِنَّهُمۡ ظَٰلِمُونَ ﴾
[آل عِمران: 128]
﴿ليس لك من الأمر شيء أو يتوب عليهم أو يعذبهم فإنهم ظالمون﴾ [آل عِمران: 128]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Huna, ewe Mtume, katika mambo ya waja chochote kile. Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Peke Yake, Asiyekuwa na mshirika. Na huenda, baadhi ya hawa waliokupiga vita, vifua vyao vikaufungukia Uislamu, wakasilimu na Mwenyezi Mungu Akazikubali toba zao. Na yule atakayesalia katika ukafiri wake, Mwenyezi Mungu Atamuadhibu duniani na Akhera kwa sababu ya udhalimu wake na uadui wake |