Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 148 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿فَـَٔاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا وَحُسۡنَ ثَوَابِ ٱلۡأٓخِرَةِۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ ﴾
[آل عِمران: 148]
﴿فآتاهم الله ثواب الدنيا وحسن ثواب الآخرة والله يحب المحسنين﴾ [آل عِمران: 148]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi Aliwapa Mwenyezi Mungu, wale wenye kusubiri, malipo yao duniani kwa kuwanusuru na maadui zao, kwa kuwafanya wakae kwa utulivu katika ardhi na kwa malipo mema yaliyo makubwa Akhera, nayo ni mabustani ya Peponi yaliyojaa neema. Na Mwenyezi Mungu Anampenda kila mtenda wema katika kumuabudu Mola wake na kuamiliana kwake na viumbe Wake |