×

Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa 3:159 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:159) ayat 159 in Swahili

3:159 Surah al-‘Imran ayat 159 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 159 - آل عِمران - Page - Juz 4

﴿فَبِمَا رَحۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ لِنتَ لَهُمۡۖ وَلَوۡ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ ٱلۡقَلۡبِ لَٱنفَضُّواْ مِنۡ حَوۡلِكَۖ فَٱعۡفُ عَنۡهُمۡ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ وَشَاوِرۡهُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِۖ فَإِذَا عَزَمۡتَ فَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَوَكِّلِينَ ﴾
[آل عِمران: 159]

Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea

❮ Previous Next ❯

ترجمة: فبما رحمة من الله لنت لهم ولو كنت فظا غليظ القلب لانفضوا, باللغة السواحيلية

﴿فبما رحمة من الله لنت لهم ولو كنت فظا غليظ القلب لانفضوا﴾ [آل عِمران: 159]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na kwa ajili ya rehema za Mwenyezi Mungu kwako na maswhaba wako, ewe Nabii, Mwenyezi Mungu Alikuneemesha ukawa laini kwao. Na lau ungalikuwa na tabia mbaya, mwenye moyo mgumu, maswahaba wako wangalijitenga na kuwa mbali na wewe. Kwa hivyo, usiwe na hasira nao kwa yaliyotokea kwao katika vita vya Uhud. Basi muombe Mwenyezi Mungu, ewe Nabii, Awasamehe na uwashauri katika mambo yanayohitajia ushauri. Na utakapoazimia kufanya jambo kati ya mambo yoyote, baada ya kushauri, litekeleze hali ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Hakika Mwenyezi Mungu Anawapenda wenye kujitegemeza Kwake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek