Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 174 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿فَٱنقَلَبُواْ بِنِعۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَضۡلٖ لَّمۡ يَمۡسَسۡهُمۡ سُوٓءٞ وَٱتَّبَعُواْ رِضۡوَٰنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ ذُو فَضۡلٍ عَظِيمٍ ﴾
[آل عِمران: 174]
﴿فانقلبوا بنعمة من الله وفضل لم يمسسهم سوء واتبعوا رضوان الله والله﴾ [آل عِمران: 174]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi wakarudi kutoka Ḥamrā’ al Asad kuja Madina wakiwa wana neema za Mwenyezi Mungu kwa kupata thawabu nyingi na nyongeza za daraja ya juu zitokazo Kwake, huku Imani na yakini zimeongezeka kwao, maadui wa Mwenyezi Mungu wamewadhalilisha, wamefaulu kwa kusalimika na kuuawa na kupigana, na wamefuata mambo ya kumridhisha Mwenyezi Mungu kwa kumtii Yeye na Mtume Wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye ihsani na vipawa vingi vyenye kuwaenea wao na wengineo |