×

Walio sema: Mwenyezi Mungu ametuahidi tusimuamini Mtume yeyote mpaka atuletee kafara inayo 3:183 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:183) ayat 183 in Swahili

3:183 Surah al-‘Imran ayat 183 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 183 - آل عِمران - Page - Juz 4

﴿ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ عَهِدَ إِلَيۡنَآ أَلَّا نُؤۡمِنَ لِرَسُولٍ حَتَّىٰ يَأۡتِيَنَا بِقُرۡبَانٖ تَأۡكُلُهُ ٱلنَّارُۗ قُلۡ قَدۡ جَآءَكُمۡ رُسُلٞ مِّن قَبۡلِي بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَبِٱلَّذِي قُلۡتُمۡ فَلِمَ قَتَلۡتُمُوهُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ﴾
[آل عِمران: 183]

Walio sema: Mwenyezi Mungu ametuahidi tusimuamini Mtume yeyote mpaka atuletee kafara inayo teketezwa na moto. Waambie: Walikujieni Mitume kabla yangu kwa hoja zilizo wazi na kwa hayo mnayo sema, basi kwa nini mkawauwa ikiwa mlikuwa wakweli

❮ Previous Next ❯

ترجمة: الذين قالوا إن الله عهد إلينا ألا نؤمن لرسول حتى يأتينا بقربان, باللغة السواحيلية

﴿الذين قالوا إن الله عهد إلينا ألا نؤمن لرسول حتى يأتينا بقربان﴾ [آل عِمران: 183]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mayahudi hawa walipoitwa kuufuata Uislamu, walisema, «Mwenyezi Mungu Ametuusia katika Taurati kwamba tusimsadiki yoyote atakayetujia na neno la kwamba yeye ni mjumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu mpaka atuletee sadaka, ambayo kwayo atajisogeza karibu na Mwenyezi Mungu, hapo ushuke moto kutoka mbinguni uiteketeze.» Sema uwaambie,ewe Mtume, «Nyinyi ni warongo kwa hayo mnayoyasema. Kwani mababa zenu kabla yangu walijiliwa na Mitume, wakiwa na hoja na dalili za ukweli wao na pia hayo mliyoyasema ya kuleta sadaka ambayo itateketezwa na moto. Basi mbona mababa zenu waliwaua Mitume hao, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu?»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek