×

Na pindi wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu, 3:20 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:20) ayat 20 in Swahili

3:20 Surah al-‘Imran ayat 20 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 20 - آل عِمران - Page - Juz 3

﴿فَإِنۡ حَآجُّوكَ فَقُلۡ أَسۡلَمۡتُ وَجۡهِيَ لِلَّهِ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡأُمِّيِّـۧنَ ءَأَسۡلَمۡتُمۡۚ فَإِنۡ أَسۡلَمُواْ فَقَدِ ٱهۡتَدَواْۖ وَّإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَٰغُۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِٱلۡعِبَادِ ﴾
[آل عِمران: 20]

Na pindi wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu, na kadhaalika walio nifuata. Na waambie walio pewa Kitabu na wasio na kisomo: Je! Mmesilimu? Wakisilimu basi wameongoka. Na wakikengeuka basi juu yako ni kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake

❮ Previous Next ❯

ترجمة: فإن حاجوك فقل أسلمت وجهي لله ومن اتبعن وقل للذين أوتوا الكتاب, باللغة السواحيلية

﴿فإن حاجوك فقل أسلمت وجهي لله ومن اتبعن وقل للذين أوتوا الكتاب﴾ [آل عِمران: 20]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wakijadiliana na wewe, ewe Mtume, Watu wa Kitabu juu ya Tawhīd: kumuwahidisha na kumpwekesha Mwenyezi Mungu, baada ya kuwasimamishia hoja, waambie, «Mimi nimemtakasia Mwenyezi Mungu Peke Yake, si mshirikishi Yeye na yoyote; na pia wale Waumini walionifuata wamemtakasia Mwenyezi Mungu na kumtii.» Na waambie wao na wale washirikina, Waarabu na wengineo, «Mkiingia kwenye Uislamu, basi nyinyi muko kwenye njia ya sawa, uongofu na haki. Na mkirudi nyuma, hesabu yenu iko kwa Mwenyezi Mungu. Mimi sina langu isipokuwa ni kufikisha ujumbe. Na mimi nimewafikishia na nimesimamisha hoja juu yenu.» Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja, hakuna chochote chenye kufichika kwake katika mambo yao
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek