×

Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio 3:19 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:19) ayat 19 in Swahili

3:19 Surah al-‘Imran ayat 19 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 19 - آل عِمران - Page - Juz 3

﴿إِنَّ ٱلدِّينَ عِندَ ٱللَّهِ ٱلۡإِسۡلَٰمُۗ وَمَا ٱخۡتَلَفَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ ﴾
[آل عِمران: 19]

Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إن الدين عند الله الإسلام وما اختلف الذين أوتوا الكتاب إلا من, باللغة السواحيلية

﴿إن الدين عند الله الإسلام وما اختلف الذين أوتوا الكتاب إلا من﴾ [آل عِمران: 19]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika dini ambayo Mwenyezi Mungu Aliwachagulia waja Wake na Akawatumiliza kwayo Mitume Wake na ambayo Hakubali isipokuwa hiyo ni Uislamu. Nao ni kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, Peke Yake, kwa kumtii na kujisalimisha Kwake kwa udhalilifu na kuwafuata Mitume katika yale waliotumilizwa kwayo katika kila kipindi mpaka wakahitimishwa kwa kuja Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ambaye, Hakubali Mwenyezi Mungu dini kutoka kwa yoyote, baada ya kutumilizwa kwake, isipokuwa Uislamu ambao alitumilizwa nao. Na tafauti baina ya Watu wa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, iliyowafanya watengane wawe mapote na makundi, haikutokea ela baada ya kuthibiti hoja juu yao kwa kupelekwa Mitume na kuteremshwa Vitabu; hiyo ilitokana na uadui na uhasidi kwa kutafuta ulimwengu.Na yoyote mwenye kuzikanusha aya za Mwenyezi Mungu zilizoteremshwa na alama Zake zenye kujulisha uola Wake na uungu Wake, basi Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa hesabu, na Atawalipa kwa yale waliokuwa wakiyafanya
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek