Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 64 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ كَلِمَةٖ سَوَآءِۭ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمۡ أَلَّا نَعۡبُدَ إِلَّا ٱللَّهَ وَلَا نُشۡرِكَ بِهِۦ شَيۡـٔٗا وَلَا يَتَّخِذَ بَعۡضُنَا بَعۡضًا أَرۡبَابٗا مِّن دُونِ ٱللَّهِۚ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقُولُواْ ٱشۡهَدُواْ بِأَنَّا مُسۡلِمُونَ ﴾
[آل عِمران: 64]
﴿قل ياأهل الكتاب تعالوا إلى كلمة سواء بيننا وبينكم ألا نعبد إلا﴾ [آل عِمران: 64]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia Watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, «Njooni kwenye neno la uadilifu na haki tushikamane nalo sote. Nalo ni sisi kuielekeza ibada yetu kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na tusimfanye yoyote kuwa ni mshirika pamoja na Yeye, awe ni sanamu au msalaba au Shetani au kinginecho. Na wala wasiwadhalilikie baadhi yetu watu wengine kwa kuwatii badala ya Mwenyezi Mungu.» Basi wakiukataa mwito huu mzuri, waambieni wao, enyi Waumini, «Kuweni ni mashahidi kwetu kuwa sisi tumejisalimisha kwa Mola wetu na tumenyosha shingo zetu Kwake kwa kukubali kuwa ni waja Wake na kwa kumtakasa.» Na mwito huu kwenye neno la sawa, kama unavyoelekezwa kwa Mayahudi na Wanaswara, unaelekezwa pia kwa wenye mwenendo kama wao |