Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 19 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿يُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَيُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّ وَيُحۡيِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَاۚ وَكَذَٰلِكَ تُخۡرَجُونَ ﴾
[الرُّوم: 19]
﴿يخرج الحي من الميت ويخرج الميت من الحي ويحي الأرض بعد موتها﴾ [الرُّوم: 19]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Anakitoa kilicho hai kutokana na kilichokufa, kama vile binadamu kutokana na tone la manii na ndege kutokana na yai, na Anakitoa kilichokufa kutokana na kilicho hai, kama vile tone la manii kutokana na binadamu na yai kutokana na ndege. Na Anahuisha ardhi kwa mimea baada ya kukauka na kuwa kavu. Na kwa namna hii ya kuhuisha mtatoka , enyi watu, makaburini mwenu mkiwa hai ili muhesabiwe na mulipwe |