Quran with Swahili translation - Surah Luqman ayat 22 - لُقمَان - Page - Juz 21
﴿۞ وَمَن يُسۡلِمۡ وَجۡهَهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِ وَهُوَ مُحۡسِنٞ فَقَدِ ٱسۡتَمۡسَكَ بِٱلۡعُرۡوَةِ ٱلۡوُثۡقَىٰۗ وَإِلَى ٱللَّهِ عَٰقِبَةُ ٱلۡأُمُورِ ﴾
[لُقمَان: 22]
﴿ومن يسلم وجهه إلى الله وهو محسن فقد استمسك بالعروة الوثقى وإلى﴾ [لُقمَان: 22]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mwenye kumtakasia Mwenyezi Mungu ibada yake na kumkusudia kwake Mola wake Aliyetukuka, na akawa mwema katika maneno yake, mwenye kutengeneza matendo yake, basi huwa ameshikamana na kamba yenye kufikisha kwenye radhi za Mwenyezi Mungu na Pepo Yake. Na kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake yanakuwa mambo yote, Akamlipa aliye mwema kwa wema wake na aliye mbaya kwa ubaya wake |