Quran with Swahili translation - Surah Luqman ayat 32 - لُقمَان - Page - Juz 21
﴿وَإِذَا غَشِيَهُم مَّوۡجٞ كَٱلظُّلَلِ دَعَوُاْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ فَلَمَّا نَجَّىٰهُمۡ إِلَى ٱلۡبَرِّ فَمِنۡهُم مُّقۡتَصِدٞۚ وَمَا يَجۡحَدُ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَّا كُلُّ خَتَّارٖ كَفُورٖ ﴾
[لُقمَان: 32]
﴿وإذا غشيهم موج كالظلل دعوا الله مخلصين له الدين فلما نجاهم إلى﴾ [لُقمَان: 32]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na washirikina wanapopanda majahazini na mawimbi makubwa yakawazunguka pambizoni mwao kama vile mawingu na majabali, huingiwa na hofu na babaiko la kuogopa kuzama, na hapo wanamkimbilia Mwenyezi Mungu na wanamtakasia dua zao, na Anapowaokoa Akawafikisha kwenye bara, kati yao kutakua na mtu wa kati na kati asiyemshukuru Mwenyezi Mungu kikamilifu, na kati yao kutakuwa na mwenye kukanusha neema za Mwenyezi Mungu na kuzikataa. Na hakanushi aya zetu na hoja zetu zenye kutolea ushahidi ukamilifu wa uweza wetu na upweke wetu isipokuwa kila mwingi wa kuvunja ahadi, mwingi wa kukataa neema za Mwenyezi Mungu juu Yake |