Quran with Swahili translation - Surah Luqman ayat 6 - لُقمَان - Page - Juz 21
﴿وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَشۡتَرِي لَهۡوَ ٱلۡحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٞ مُّهِينٞ ﴾
[لُقمَان: 6]
﴿ومن الناس من يشتري لهو الحديث ليضل عن سبيل الله بغير علم﴾ [لُقمَان: 6]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa watu kuna anayenunua maneno ya pumbao, nayo ni kila chenye kumpumbaza mtu na utiifu wa Mwenyezi Mungu, ili awapoteze watu na njia ya uongofu wafuate njia ya matamanio na azifanye aya za Mwenyezi Mungu kuwa ni shere, basi hao watakuwa na adhabu yenye kuwadhalilisha na kuwatweza |