Quran with Swahili translation - Surah As-Sajdah ayat 3 - السَّجدة - Page - Juz 21
﴿أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۚ بَلۡ هُوَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوۡمٗا مَّآ أَتَىٰهُم مِّن نَّذِيرٖ مِّن قَبۡلِكَ لَعَلَّهُمۡ يَهۡتَدُونَ ﴾
[السَّجدة: 3]
﴿أم يقولون افتراه بل هو الحق من ربك لتنذر قوما ما أتاهم﴾ [السَّجدة: 3]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani je, wanasema washirikina kuwa Muhammad Ameizua Qur’ani? Wamesema urongo, bali hiyo Qur’ani ndiyo ukweli uliothibiti ulioteremshwa kwako, ewe Mtume, kutoka kwa Mola wako, ili uwaonye nayo watu ambao hawakujiwa na muonyaji kabla yako wewe, huenda wao wakaongoka: wakaijua haki, wakaiamini, wakaitanguliza na wakakuamini wewe |