×

Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao 32:4 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah As-Sajdah ⮕ (32:4) ayat 4 in Swahili

32:4 Surah As-Sajdah ayat 4 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah As-Sajdah ayat 4 - السَّجدة - Page - Juz 21

﴿ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ مَا لَكُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَلِيّٖ وَلَا شَفِيعٍۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ ﴾
[السَّجدة: 4]

Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa siku sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki

❮ Previous Next ❯

ترجمة: الله الذي خلق السموات والأرض وما بينهما في ستة أيام ثم استوى, باللغة السواحيلية

﴿الله الذي خلق السموات والأرض وما بينهما في ستة أيام ثم استوى﴾ [السَّجدة: 4]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu Ndiye Ambaye aliumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina yake kwa Siku sita kwa hekima Anayoijua. Na Yeye ni Muweza wa kuziumba kwa neno «Kuwa» na likawa, kisha Akalingana, Kutakasika na kuwa juu ni Kwake - nako ni kuwa juu na kunyanyuka- juu ya ‘Arsh Yake , kulingana kunakonasibiana na utukufu Wake, hakusemwi kuko namna gani wala hakufananishwi na vile binadamu wanavyolingana. Hamna nyinyi, enyi watu, mtegemewa wa kumtegemezea mambo yenu, au muombezi wa kuwaombea nyinyi mbele ya Mwenyezi Mungu, ili muokoke na adhabu Yake. Basi kwani nyinyi hamwaidhiki na mkafikiria, enyi watu, mkampwekesha Mwenyezi Mungu kwa uungu na mkamtakasia ibada
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek