Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 16 - الأحزَاب - Page - Juz 21
﴿قُل لَّن يَنفَعَكُمُ ٱلۡفِرَارُ إِن فَرَرۡتُم مِّنَ ٱلۡمَوۡتِ أَوِ ٱلۡقَتۡلِ وَإِذٗا لَّا تُمَتَّعُونَ إِلَّا قَلِيلٗا ﴾
[الأحزَاب: 16]
﴿قل لن ينفعكم الفرار إن فررتم من الموت أو القتل وإذا لا﴾ [الأحزَاب: 16]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Nabii, kuwaambia hawa wanafiki, «Kukimbia kwenu vitani kwa kuogopa kufa au kuuawa, huko hakutachelewesha muda wenu wa kuishi katika dunia hii, na mkikimbia hamtastarehe katika dunia hii isipokuwa kwa kadiri ya umri wenu uliowekewa kikomo, nacho ni muda mchache sana ukilinganishwa na Akhera.» |