Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 25 - الأحزَاب - Page - Juz 21
﴿وَرَدَّ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِغَيۡظِهِمۡ لَمۡ يَنَالُواْ خَيۡرٗاۚ وَكَفَى ٱللَّهُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٱلۡقِتَالَۚ وَكَانَ ٱللَّهُ قَوِيًّا عَزِيزٗا ﴾
[الأحزَاب: 25]
﴿ورد الله الذين كفروا بغيظهم لم ينالوا خيرا وكفى الله المؤمنين القتال﴾ [الأحزَاب: 25]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Akayarudisha Mwenyezi Mungu mapote ya ukafiri kutoka Madina yakiwa yamepita patupu, yamepata hasara na yamejawa na hasira, hayakupata kheri yoyote duniani wala Akhera, na Mwenyezi Mungu Akawatosheleza Waumini (wasilazimike) kupigana kwa kuwasaidia kwa sababu Alizowatolea. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Hashindwi wala Halazimishwi, ni Mshindi katika ufalme Wake na mamlaka Yake |