Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 24 - الأحزَاب - Page - Juz 21
﴿لِّيَجۡزِيَ ٱللَّهُ ٱلصَّٰدِقِينَ بِصِدۡقِهِمۡ وَيُعَذِّبَ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ إِن شَآءَ أَوۡ يَتُوبَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا ﴾
[الأحزَاب: 24]
﴿ليجزي الله الصادقين بصدقهم ويعذب المنافقين إن شاء أو يتوب عليهم إن﴾ [الأحزَاب: 24]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ili Mwenyezi Mungu Awalipe mema watu wa ukweli kwa ukweli wao na kujitolea kwao, nao ni Waumini, na ili Awaadhibu wanafiki Akitaka kuwaadhibu, kwa kutowapa taufiki ya kutubia toba ya kidhati kabla ya kufa, hivyo basi wafe kwenye ukafiri na wastahili Moto, au Awape taufiki ya kutubia na kurejea, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe dhambi za wenye kuzidhulumu nafsi zao, ni Mwingi wa huruma kwao kwa kuwapa taufiki ya kutubia toba ya kidhati |