Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 27 - الأحزَاب - Page - Juz 21
﴿وَأَوۡرَثَكُمۡ أَرۡضَهُمۡ وَدِيَٰرَهُمۡ وَأَمۡوَٰلَهُمۡ وَأَرۡضٗا لَّمۡ تَطَـُٔوهَاۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٗا ﴾
[الأحزَاب: 27]
﴿وأورثكم أرضهم وديارهم وأموالهم وأرضا لم تطئوها وكان الله على كل شيء﴾ [الأحزَاب: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Akawamilikisha nyinyi, enyi Waumini, ardhi yao, makazi yao na mali yao yanayohamishika kama vile pambo, silaha na wanyama na yasiyohamishika kama vile mashamba, nyumba na ngome zilizojikita. Na Akawarithisha ardhi ambayo hamkuweza kuikanyaga kabla ya hapo. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu, hakuna kinachomshinda |