Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 28 - الأحزَاب - Page - Juz 21
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ قُل لِّأَزۡوَٰجِكَ إِن كُنتُنَّ تُرِدۡنَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيۡنَ أُمَتِّعۡكُنَّ وَأُسَرِّحۡكُنَّ سَرَاحٗا جَمِيلٗا ﴾
[الأحزَاب: 28]
﴿ياأيها النبي قل لأزواجك إن كنتن تردن الحياة الدنيا وزينتها فتعالين أمتعكن﴾ [الأحزَاب: 28]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ewe Nabii! Waambie wake zako waliojikusanya mbele yako wakitaka kwako ongezo la matumizi, «Mkiwa mnataka maisha ya kilimwengu na pambo lake, basi njooni niwastareheshe kwa kitu kichache cha kilimwengu nilicho nacho na niwatenge bila ya kuwadhuru wala kuwaudhi |