Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 55 - الأحزَاب - Page - Juz 22
﴿لَّا جُنَاحَ عَلَيۡهِنَّ فِيٓ ءَابَآئِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآئِهِنَّ وَلَآ إِخۡوَٰنِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآءِ إِخۡوَٰنِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآءِ أَخَوَٰتِهِنَّ وَلَا نِسَآئِهِنَّ وَلَا مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُنَّۗ وَٱتَّقِينَ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدًا ﴾
[الأحزَاب: 55]
﴿لا جناح عليهن في آبائهن ولا أبنائهن ولا إخوانهن ولا أبناء إخوانهن﴾ [الأحزَاب: 55]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakuna dhambi kwa wanawake kutojifinika mbele ya baba zao, wana wao wa kiume,ndugu zao wa kiume, wana wa kiume wa ndugu zao wa kiume, wana wa kiume wa ndugu zao wa kike, wanawake waumini na watumwa waliomilikiwa na wao kwa kuwa wanahitaji utumishi wao sana. Na muogopeni Mwenyezi Mungu , enyi wanawake, msipite mpaka mliowekewa mkaonyesha pambo lenu msiofaa kulionyesha, au mkaacha kujifinika mbele ya yule ambaye ni lazima mjifinike mbele yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu, Anashuhudia matendo ya waja , ya nje na ya ndani, na Atawalipa kwayo |