Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 56 - الأحزَاب - Page - Juz 22
﴿إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِيِّۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ صَلُّواْ عَلَيۡهِ وَسَلِّمُواْ تَسۡلِيمًا ﴾
[الأحزَاب: 56]
﴿إن الله وملائكته يصلون على النبي ياأيها الذين آمنوا صلوا عليه وسلموا﴾ [الأحزَاب: 56]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika Mwenyezi Mungu Anamsifu Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, mbele ya Malaika waliokurubishwa. Na Malaika Wake wanamsifu Nabii na wanamuombea Mwenyezi Mungu, basi enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, mswalieni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mtakieni amani, kwa kumwamkia na kumtukuza. Na namna ya kumswalia Nabii, rehema na amani zimshukie, imethibiti kwenye Sunnah kwa aina mabalimbali, miongoni mwazo ni: «Ewe Mola! Mrehemu Muhammad na watu wa Muhammad, kama ulivyowarehemu watu wa Ibrāhīm, hakika wewe ni Mwingi wa kushukuriwa ni Mwingi wa kutukuzwa. Ewe Mola! Mbariki Muhammad na watu wa Muhammad kama ulivyowabariki watu wa Ibrāhīm, hakika wewe ni Mwingi wa kushukuriwa, ni Mwingi wa kutukuzwa.» |