Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 13 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿يَعۡمَلُونَ لَهُۥ مَا يَشَآءُ مِن مَّحَٰرِيبَ وَتَمَٰثِيلَ وَجِفَانٖ كَٱلۡجَوَابِ وَقُدُورٖ رَّاسِيَٰتٍۚ ٱعۡمَلُوٓاْ ءَالَ دَاوُۥدَ شُكۡرٗاۚ وَقَلِيلٞ مِّنۡ عِبَادِيَ ٱلشَّكُورُ ﴾
[سَبإ: 13]
﴿يعملون له ما يشاء من محاريب وتماثيل وجفان كالجواب وقدور راسيات اعملوا﴾ [سَبإ: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Majini wanamfanyia Sulaymān anachotaka miongoni mwa misikiti ya ibada, picha za shaba na ukoa, madishi makubwa kama mabirika ya kukusanyika maji ndani yake na vyungu vilivyojikita visivyotikisika kutoka mahali pake kwa ukubwa wake, na tukasema, «Enyi jamii ya Dāwūd! Fanyeni kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kile Alichowapa, kwa kumtii na kufuata amri Yake.» Na ni wachache, miongoni mwa waja wangu, wenye kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi. Na Dāwūd, yeye na jamii yake, alikuwa miongoni mwa hao wachache |