Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 12 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿وَلِسُلَيۡمَٰنَ ٱلرِّيحَ غُدُوُّهَا شَهۡرٞ وَرَوَاحُهَا شَهۡرٞۖ وَأَسَلۡنَا لَهُۥ عَيۡنَ ٱلۡقِطۡرِۖ وَمِنَ ٱلۡجِنِّ مَن يَعۡمَلُ بَيۡنَ يَدَيۡهِ بِإِذۡنِ رَبِّهِۦۖ وَمَن يَزِغۡ مِنۡهُمۡ عَنۡ أَمۡرِنَا نُذِقۡهُ مِنۡ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ ﴾
[سَبإ: 12]
﴿ولسليمان الريح غدوها شهر ورواحها شهر وأسلنا له عين القطر ومن الجن﴾ [سَبإ: 12]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tulimdhalilishia Sulaymān upepo, ukawa unatembea kutoka mwanzo wa mchana mpaka katikati yake mwendo wa mwezi, na kutoka katikati ya mchana mpaka usiku mwendo wa mwezi kwa mwendo wa kawaida. Na tulimyayushia shaba ikawa inatiririka kama vile maji yanavyotiririka, akawa anafanya kwa shaba hiyo anachotaka. Na tulimdhalilishia miongoni mwa majini wenye kutumika mbele yake, na yoyote kati yao anayesita kufuata amri yetu tuliomuamrisha ya kumtii Sulaymān tutamuonjesha kutokana na adhabu ya Moto unaowaka |