Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 27 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿قُلۡ أَرُونِيَ ٱلَّذِينَ أَلۡحَقۡتُم بِهِۦ شُرَكَآءَۖ كـَلَّاۚ بَلۡ هُوَ ٱللَّهُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ﴾
[سَبإ: 27]
﴿قل أروني الذين ألحقتم به شركاء كلا بل هو الله العزيز الحكيم﴾ [سَبإ: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, «Nionesheni kwa hoja na dalili wale mliomshikanisha na Mwenyezi Mungu mkawafanya ni washirika Wake katika kuabudiwa, je wao wameumba chochote? Mambo si kama walivyoeleza.Bali Yeye Ndiye Mwenye kuabudiwa kwa haki, ambaye hana mshirika wake, aliye Mshindi katika kuwatesa waliomshirikisha, na mwenye hekima katika maneno Yake, vitendo Vyake na upelekeshaji mambo ya viumbe Vyake |