Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 9 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿أَفَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَىٰ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِۚ إِن نَّشَأۡ نَخۡسِفۡ بِهِمُ ٱلۡأَرۡضَ أَوۡ نُسۡقِطۡ عَلَيۡهِمۡ كِسَفٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّكُلِّ عَبۡدٖ مُّنِيبٖ ﴾
[سَبإ: 9]
﴿أفلم يروا إلى ما بين أيديهم وما خلفهم من السماء والأرض إن﴾ [سَبإ: 9]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hawaoni makafiri hawa wasioamini Akhera ukubwa wa uweza wa Mwenyezi Mungu juu ya vilivyoko mbele yao na nyuma yao, miongoni mwa mbingu na ardhi, vinavyoshangaza akili, na kwamba viwili hivyo vimewazunguka? Tutakapo tutawazamisha ndani ya ardhi, kama tulivyomfanyia Qārūn, au tutawateremshia vipande vya adhabu, kama tulivyowafanyia watu wa Shu'ayb, kwa hakika mbingu iliwanyeshea moto ukawaunguza. Hakika katika hilo tulilolitaja la uwezo wetu kuna ushahidi wazi kwa kila mja mwenye kurudi kwa Mola wao kwa kutubia, mwenye kukubali upweke Wake na mwenye kumtakasia ibada |