Quran with Swahili translation - Surah Ya-Sin ayat 33 - يسٓ - Page - Juz 23
﴿وَءَايَةٞ لَّهُمُ ٱلۡأَرۡضُ ٱلۡمَيۡتَةُ أَحۡيَيۡنَٰهَا وَأَخۡرَجۡنَا مِنۡهَا حَبّٗا فَمِنۡهُ يَأۡكُلُونَ ﴾
[يسٓ: 33]
﴿وآية لهم الأرض الميتة أحييناها وأخرجنا منها حبا فمنه يأكلون﴾ [يسٓ: 33]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na ili kuwaonyesha hawa washirikina ushahidi wa uweza wa Mwenyezi Mungu wa kufufua na kukusanya ni hii ardhi iliyokufa isiyo na mimea, tumeihuisha kwa kuteremsha maji, na tukatoa humo aina mbalimbali za mimea ambayo watu na wanyama wanakula. Na Mwenye kuhuisha ardhi kwa mimea Ndiye Atakayehuisha viumbe baada ya kufa |