Quran with Swahili translation - Surah sad ayat 24 - صٓ - Page - Juz 23
﴿قَالَ لَقَدۡ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعۡجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِۦۖ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلۡخُلَطَآءِ لَيَبۡغِي بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٍ إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَقَلِيلٞ مَّا هُمۡۗ وَظَنَّ دَاوُۥدُ أَنَّمَا فَتَنَّٰهُ فَٱسۡتَغۡفَرَ رَبَّهُۥ وَخَرَّۤ رَاكِعٗاۤ وَأَنَابَ۩ ﴾
[صٓ: 24]
﴿قال لقد ظلمك بسؤال نعجتك إلى نعاجه وإن كثيرا من الخلطاء ليبغي﴾ [صٓ: 24]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Dāwūd akasema, «Kwa hakika ndugu yako amekudhulumu kwa kutaka kwake kumchukua kondoo wako awe pamoja na kondoo wake. Na kwa hakika, wengi wa washirika, baadhi yao wanadhulumu wengine: wanawadhulumu kwa kuchukua haki zao na kukosa kuwa waadilifu wa nafsi zao. Isipokuwa watu wema walioamini, kwani wao hawadhulumiani, nao ni wachache.» Na Dāwūd akajua kwa yakini kuwa sisi tumemtahini kwa utesi huu, hivyo basi akamuomba msamaha Mola wake, akasujudu kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na akarejea Kwake na akatubia |