Quran with Swahili translation - Surah sad ayat 34 - صٓ - Page - Juz 23
﴿وَلَقَدۡ فَتَنَّا سُلَيۡمَٰنَ وَأَلۡقَيۡنَا عَلَىٰ كُرۡسِيِّهِۦ جَسَدٗا ثُمَّ أَنَابَ ﴾
[صٓ: 34]
﴿ولقد فتنا سليمان وألقينا على كرسيه جسدا ثم أناب﴾ [صٓ: 34]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika tulimpa mtihani Sulaymān na tukamrushia kwenye kiti chake kipande cha mtoto aliyezaliwa katika kipindi alichoapa kuwa atawapitia wake zake na kila mmoja katika wao atamzalia shujaa atakayepigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, na hakuseme «in shāa Allāh» (Mungu Akitaka). Akawapitia wake zake wote, na hakuna hata mmoja katika wao aliyeshika mimba isipokuwa mmoja aliyezaa mtoto nusu. Kisha Sulaymān alirudi kwa Mola Wake, akatubia |