Quran with Swahili translation - Surah sad ayat 72 - صٓ - Page - Juz 23
﴿فَإِذَا سَوَّيۡتُهُۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُواْ لَهُۥ سَٰجِدِينَ ﴾
[صٓ: 72]
﴿فإذا سويته ونفخت فيه من روحي فقعوا له ساجدين﴾ [صٓ: 72]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi nitakapousawazisha mwili wake na umbo lake na nikapuliza roho ndani yake na uhai ukatambaa humo, msujudieni» sijida ya heshima na kukirimu, na siyo sijida ya ibada na kutukuza. Kwani ibada haiwi isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Na Mwenyezi Mungu Ameharamisha, katika Sheria ya Kiislamu, kusujudu kwa njia ya maamkizi |