Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 21 - الزُّمَر - Page - Juz 23
﴿أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَسَلَكَهُۥ يَنَٰبِيعَ فِي ٱلۡأَرۡضِ ثُمَّ يُخۡرِجُ بِهِۦ زَرۡعٗا مُّخۡتَلِفًا أَلۡوَٰنُهُۥ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَىٰهُ مُصۡفَرّٗا ثُمَّ يَجۡعَلُهُۥ حُطَٰمًاۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكۡرَىٰ لِأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ ﴾
[الزُّمَر: 21]
﴿ألم تر أن الله أنـزل من السماء ماء فسلكه ينابيع في الأرض﴾ [الزُّمَر: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, huoni, ewe Mtume, kuwa Mwenyezi Mungu Anateremsha mvua kutoka mawinguni, akaitia ardhini, akaifanya ni mikondo yenye kuchimbuka na maji yenye kutiririka, kisha anatoa kwa maji hayo mimea yenye rangi tafauti na aina mbalimbali, kisha inakauka baada ya ubichi wake na mng’aro wake, hapo utaiona imebadilika kuwa rangi ya manjano, kisha Anaifanya kuwa ni mapepe yaliyovunjikavunjika na kumumunyuka? Kwa hakika, katika kitendo hiko cha Mwenyezi Mungu pana ukumbusho na mawaidha kwa wenye akili timamu |