×

Na ukiwauliza: Ni nani aliye ziumba mbingu na ardhi. Bila ya shaka 39:38 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Az-Zumar ⮕ (39:38) ayat 38 in Swahili

39:38 Surah Az-Zumar ayat 38 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 38 - الزُّمَر - Page - Juz 24

﴿وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّنۡ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُۚ قُلۡ أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ إِنۡ أَرَادَنِيَ ٱللَّهُ بِضُرٍّ هَلۡ هُنَّ كَٰشِفَٰتُ ضُرِّهِۦٓ أَوۡ أَرَادَنِي بِرَحۡمَةٍ هَلۡ هُنَّ مُمۡسِكَٰتُ رَحۡمَتِهِۦۚ قُلۡ حَسۡبِيَ ٱللَّهُۖ عَلَيۡهِ يَتَوَكَّلُ ٱلۡمُتَوَكِّلُونَ ﴾
[الزُّمَر: 38]

Na ukiwauliza: Ni nani aliye ziumba mbingu na ardhi. Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Sema: Je! Mnawaonaje wale mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondolea dhara yake? Au akitaka kunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake? Sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Kwake Yeye wategemee wanao tegemea

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ولئن سألتهم من خلق السموات والأرض ليقولن الله قل أفرأيتم ما تدعون, باللغة السواحيلية

﴿ولئن سألتهم من خلق السموات والأرض ليقولن الله قل أفرأيتم ما تدعون﴾ [الزُّمَر: 38]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na unapowauliza, ewe Mtume, hawa washirikina wanaomuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, «Ni nani aliyeziumba hizi mbingu na ardhi?» watasema, «Aliyeziumba ni Mwenyezi Mungu.» Kwa hivyo wao wanamkubali Muumba. Basi waambie, «Je, waungu hawa mnaowashirikisha na Mwenyezi Mungu wanaweza kuniepushia makero ambayo Mwenyezi Mungu Amenikadiria au kuniondolea mambo ninayoyachukia yaliyonifika? Na je, wanaweza wao kuzuia manufaa aliyonisahilishia Mwenyezi Mungu nisiyapate au kunizuilia rehema ya Mwenyezi Mungu isinifikie?» Wao watasema, «Hawawezi hilo.» Waambie, «Mwenye kunitosheleza na kuniridhisha mimi ni Mwenyezi Mungu. Kwake yeye wanategemea wenye kutegemea katika kuleta yanayowafaa na kuzuia yanayowadhuru. Yule ambaye kwenye mkono wake peke yake kuna toshelezo, Yeye Ndiye Mwenye kunitosha na Atanikifia kila linalonitia hamu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek