×

Na mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu atapata pengi duniani pa 4:100 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:100) ayat 100 in Swahili

4:100 Surah An-Nisa’ ayat 100 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 100 - النِّسَاء - Page - Juz 5

﴿۞ وَمَن يُهَاجِرۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ يَجِدۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُرَٰغَمٗا كَثِيرٗا وَسَعَةٗۚ وَمَن يَخۡرُجۡ مِنۢ بَيۡتِهِۦ مُهَاجِرًا إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ يُدۡرِكۡهُ ٱلۡمَوۡتُ فَقَدۡ وَقَعَ أَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا ﴾
[النِّسَاء: 100]

Na mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na anaye toka nyumbani kwake kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti njiani basi umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ومن يهاجر في سبيل الله يجد في الأرض مراغما كثيرا وسعة ومن, باللغة السواحيلية

﴿ومن يهاجر في سبيل الله يجد في الأرض مراغما كثيرا وسعة ومن﴾ [النِّسَاء: 100]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na yoyote mwenye kutoka kwenye ardhi ya ushirikina kwenda kwenye ardhi ya Uislamu kwa ajili ya kukimbia na dini Yake, akitaraji fadhila za Mola wake na akikusudia kuinusuru dini Yake, atapata katika ardhi mahali pa kuelekea ambapo ataneemeka, pawe ni sababu ya yeye kupata nguvu na maadui zake kuwa wanyonge, pamoja na kupata ukunjufu wa riziki na maisha. Na yoyote mwenye kutoka nyumbani kwake kwa lengo la kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye na kulitukuza neno la Mwenyezi Mungu kisha akapatikana na kifo kabla ya kufikia lengo lake, basi malipo ya kitendo chake yameshathibiti kwa Mwenyezi Mungu, kwa fadhila Zake na wema Wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, ni Mwingi wa huruma kwa waja Wake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek