Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 101 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَإِذَا ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَقۡصُرُواْ مِنَ ٱلصَّلَوٰةِ إِنۡ خِفۡتُمۡ أَن يَفۡتِنَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْۚ إِنَّ ٱلۡكَٰفِرِينَ كَانُواْ لَكُمۡ عَدُوّٗا مُّبِينٗا ﴾
[النِّسَاء: 101]
﴿وإذا ضربتم في الأرض فليس عليكم جناح أن تقصروا من الصلاة إن﴾ [النِّسَاء: 101]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mnaposafiri, enyi Waumini, kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, hamuna makosa wala dhambi kukupunguza Swala, mkiogopa kufanyiwa uadui na makafiri mkiwa kwenye Swala. Safari nyinygi za Waislamu, katika mwanzo wa Uislamu, zilikuwa za kutisha. Na kupunguza Swala ni ruhusa iliyotolewa kwenye safari, katika hali ya amani au vitisho. Hakika makafiri ni wenye kudhihirisha uadui wao kwenu, basi jihadharini nao |