Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 102 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَإِذَا كُنتَ فِيهِمۡ فَأَقَمۡتَ لَهُمُ ٱلصَّلَوٰةَ فَلۡتَقُمۡ طَآئِفَةٞ مِّنۡهُم مَّعَكَ وَلۡيَأۡخُذُوٓاْ أَسۡلِحَتَهُمۡۖ فَإِذَا سَجَدُواْ فَلۡيَكُونُواْ مِن وَرَآئِكُمۡ وَلۡتَأۡتِ طَآئِفَةٌ أُخۡرَىٰ لَمۡ يُصَلُّواْ فَلۡيُصَلُّواْ مَعَكَ وَلۡيَأۡخُذُواْ حِذۡرَهُمۡ وَأَسۡلِحَتَهُمۡۗ وَدَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡ تَغۡفُلُونَ عَنۡ أَسۡلِحَتِكُمۡ وَأَمۡتِعَتِكُمۡ فَيَمِيلُونَ عَلَيۡكُم مَّيۡلَةٗ وَٰحِدَةٗۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ إِن كَانَ بِكُمۡ أَذٗى مِّن مَّطَرٍ أَوۡ كُنتُم مَّرۡضَىٰٓ أَن تَضَعُوٓاْ أَسۡلِحَتَكُمۡۖ وَخُذُواْ حِذۡرَكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ أَعَدَّ لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا ﴾
[النِّسَاء: 102]
﴿وإذا كنت فيهم فأقمت لهم الصلاة فلتقم طائفة منهم معك وليأخذوا أسلحتهم﴾ [النِّسَاء: 102]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na ukiwa, ewe Nabii, kwenye kiwanja cha vita na ukataka kuswalisha, basi kundi moja lisimame nawe ili kuswali, huku wakiwa wameshika silaha zao. Watu wa kundi hili wakiwa kwenye sijda, basi lije kundi lingine liwe nyuma yenu likiwa limeelekea upande wa adui wenu. Watu wa kundi la kwanza watimize rakaa ya pili na kutoa salamu. Kisha watu wa kundi lingine, ambalo bado halijaanza kuswali, waje kukufuata katika rakaa yao ya kwanza, kisha wamalize wenyewe rakaa yao ya pili. Na wajihadhari na adui wao na washike silaha zao. Kwani wenye kukanusha dini ya Mwenyezi Mungu wanatamani mughafilike na silaha zenu na vyombo vyenu wapate kuwashambulia kwa mara moja na kuwaua. Na hamuna makosa, kukiwa na mvua yenye kuwasumbua au mkawa wagonjwa, kuaacha silaha zenu pamoja na kuwa na hadhari. Hakika Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Amewaandalia wenye kuikanusha dini Yake adhabu ya kuwatweza na kuwadhalilisha |