Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 113 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ وَرَحۡمَتُهُۥ لَهَمَّت طَّآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡۖ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَيۡءٖۚ وَأَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمۡ تَكُن تَعۡلَمُۚ وَكَانَ فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ عَظِيمٗا ﴾
[النِّسَاء: 113]
﴿ولولا فضل الله عليك ورحمته لهمت طائفة منهم أن يضلوك وما يضلون﴾ [النِّسَاء: 113]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau si Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kukuneemesha, ewe Mtume, kukurehemu kwa neema ya unabii na kukuhifadhi, kwa taufiki Yake, kwa wahyi Aliokuletea, wangaliazimia watu, miongoni mwa wale wanaozifanyia hiana nafsi zao, kukupotosha na njia ya haki. Na wao kwa kufanya hivyo, huwa hawampotoshi yoyote isipokuwa nafsi zao. Na hawawezi kukudhuru kwa kuwa Mwenyezi Mungu Amekuhifadhi, Amekuteremshia Qur’ani na Sunnah yenye kuifafanua, na Amekuongoza ukajua elimu ambayo hukuwa ukiijua hapo nyuma. Na fadhila za Mwenyezi Mungu Alizokuhusisha nazo ni jambo kubwa |