Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 122 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ سَنُدۡخِلُهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٗاۚ وَمَنۡ أَصۡدَقُ مِنَ ٱللَّهِ قِيلٗا ﴾
[النِّسَاء: 122]
﴿والذين آمنوا وعملوا الصالحات سندخلهم جنات تجري من تحتها الأنهار خالدين فيها﴾ [النِّسَاء: 122]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wale waliokuwa wakweli katika kumuamini kwao Mwenyezi Mungu, Aliyetukua, na wakafuatanisha Imani yao na matendo mema, basi Mwenyezi Mungu Atawaingiza, kwa ukarimu Wake, ndani ya mabustani ya Pepo ambayo chini ya majumba yake ya fahari na miti yake inapita mito, hali ya kukaa milele humo. Hiyo ni ahadi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ambaye Haendi kinyume na ahadi Yake. Na hapana yoyote aliye mkweli zaidi, katika neno lake na ahadi yake, kuliko Mwenyezi Mungu Aliyetukuka |