Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 123 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿لَّيۡسَ بِأَمَانِيِّكُمۡ وَلَآ أَمَانِيِّ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِۗ مَن يَعۡمَلۡ سُوٓءٗا يُجۡزَ بِهِۦ وَلَا يَجِدۡ لَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا ﴾
[النِّسَاء: 123]
﴿ليس بأمانيكم ولا أماني أهل الكتاب من يعمل سوءا يجز به ولا﴾ [النِّسَاء: 123]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Fadhila hizi kubwa hazipatikani kwa matamanio mnayoyatamani, enyi Waislamu, wala kwa matamanio ya Mayahudi na Wanaswara waliopewa Kitabu. Hakika zinapatikana kwa kumuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kikweli na kuyafanya vizuri matendo ya kumridhisha. Na yoyote mwenye kufanya tendo baya, atalipwa kwalo, na hatompata, asiyekuwa Mwenyezi Mungu, mtegemewa mwenye kusimamia mambo yake wala msaidizi mwenye kumnusuru na kumuepushia adhabu mbaya |