Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 130 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغۡنِ ٱللَّهُ كُلّٗا مِّن سَعَتِهِۦۚ وَكَانَ ٱللَّهُ وَٰسِعًا حَكِيمٗا ﴾
[النِّسَاء: 130]
﴿وإن يتفرقا يغن الله كلا من سعته وكان الله واسعا حكيما﴾ [النِّسَاء: 130]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na ukitokea utengano baina ya mwanamume na mkewe, Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, atamtosheleza kila mmoja kati yao kwa fadhila Zake na ukunjufu wa neema Zake. Kwani Yeye, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu na Aliyetukuka, ni Mkunjufu wa fadhila na neema, ni Mwingi wa hekima katika hukumu Zake Anazozipitisha kwa waja Wake |