×

Wale ambao wanakungojeeni, mkipata ushindi unao toka kwa Mwenyezi Mungu wao husema: 4:141 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:141) ayat 141 in Swahili

4:141 Surah An-Nisa’ ayat 141 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 141 - النِّسَاء - Page - Juz 5

﴿ٱلَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمۡ فَإِن كَانَ لَكُمۡ فَتۡحٞ مِّنَ ٱللَّهِ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَكُن مَّعَكُمۡ وَإِن كَانَ لِلۡكَٰفِرِينَ نَصِيبٞ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَسۡتَحۡوِذۡ عَلَيۡكُمۡ وَنَمۡنَعۡكُم مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ فَٱللَّهُ يَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَلَن يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لِلۡكَٰفِرِينَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ سَبِيلًا ﴾
[النِّسَاء: 141]

Wale ambao wanakungojeeni, mkipata ushindi unao toka kwa Mwenyezi Mungu wao husema: Si tulikuwa pamoja nanyi vile? Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda wao huwaambia: Hatukuwa ni waweza wa kukushindeni, nasi tukakukingeni na hawa Waumini? Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini

❮ Previous Next ❯

ترجمة: الذين يتربصون بكم فإن كان لكم فتح من الله قالوا ألم نكن, باللغة السواحيلية

﴿الذين يتربصون بكم فإن كان لكم فتح من الله قالوا ألم نكن﴾ [النِّسَاء: 141]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wanafiki ndio wale wanaongojea yatakayowashukia nyinyi, enyi Waumini, ya misukosuko na vita. Iwapo Mwenyezi Mungu Amewaneemesha kwa fadhila Zake, Akawanusuru juu ya adui yenu na mkapata ngawira, wao wanasema, «Kwani hatukuwa na nyinyi tukiwasaidia?» Na iwapo wakanushaji wa Dini hii wamepata sehemu ya ushindi na ngawira, wao wanasema kuwaambia, «Kwani hatukuwasaidia nyinyi kwa kile tulichowapatia na kuwahami na Waumini?» Basi Mwenyezi Mungu Ataamua baina yao na nyinyi Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu Hatawapa makafiri njia ya kuwashinda waja Wake wema. Basi mwisho mwema ni wa wacha- Mungu, duniani na Akhera
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek