Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 143 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿مُّذَبۡذَبِينَ بَيۡنَ ذَٰلِكَ لَآ إِلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِ وَلَآ إِلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِۚ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلٗا ﴾
[النِّسَاء: 143]
﴿مذبذبين بين ذلك لا إلى هؤلاء ولا إلى هؤلاء ومن يضلل الله﴾ [النِّسَاء: 143]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hali ya hawa wanafiki ni kutokuwa na msimamo, kuchangayikiwa na kubabaika, hawathibiti kwenye hali moja, hawako pamoja na Waumini wala hawako pamoja na makafiri. Na yoyote ambaye Mwenyezi Mungu Ameupotoa moyo wake usimuamini na usishikamane na uongofu Wake, huyo hutampatia njia ya kufikia uongofu na yakini |