×

Wanakuomba uhukumu, sema: Mwenyezi Mungu anakupeni hukumu juu ya mkiwa. Ikiwa mtu 4:176 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:176) ayat 176 in Swahili

4:176 Surah An-Nisa’ ayat 176 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 176 - النِّسَاء - Page - Juz 6

﴿يَسۡتَفۡتُونَكَ قُلِ ٱللَّهُ يُفۡتِيكُمۡ فِي ٱلۡكَلَٰلَةِۚ إِنِ ٱمۡرُؤٌاْ هَلَكَ لَيۡسَ لَهُۥ وَلَدٞ وَلَهُۥٓ أُخۡتٞ فَلَهَا نِصۡفُ مَا تَرَكَۚ وَهُوَ يَرِثُهَآ إِن لَّمۡ يَكُن لَّهَا وَلَدٞۚ فَإِن كَانَتَا ٱثۡنَتَيۡنِ فَلَهُمَا ٱلثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَۚ وَإِن كَانُوٓاْ إِخۡوَةٗ رِّجَالٗا وَنِسَآءٗ فَلِلذَّكَرِ مِثۡلُ حَظِّ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۗ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ أَن تَضِلُّواْۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ ﴾
[النِّسَاء: 176]

Wanakuomba uhukumu, sema: Mwenyezi Mungu anakupeni hukumu juu ya mkiwa. Ikiwa mtu amekufa, naye hana mtoto, lakini anaye ndugu wa kike, basi huyo atapata nusu alicho acha maiti. Na mwanamume atamrithi ndugu wa kike ikiwa hana mwana. Na ikiwa wao ni ndugu wa kike wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho acha maiti. Na wakiwa ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamume atapata sehemu iliyo sawa na ya wanawake wawili. Mwenyezi Mungu anakubainishieni ili msipotee; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: يستفتونك قل الله يفتيكم في الكلالة إن امرؤ هلك ليس له ولد, باللغة السواحيلية

﴿يستفتونك قل الله يفتيكم في الكلالة إن امرؤ هلك ليس له ولد﴾ [النِّسَاء: 176]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wanakuuliza, ewe Nabii, kuhusu hukumu ya urithi wa kalalah, naye ni aliyekufa akiwa hana mwana wala mzazi. Sema, «Mwenyezi Mungu Anawafafanulia hukumu yake, kwamba yoyote atakayefariki na akawa hana mwana wala mzazi, na akawa ana dada yake wa kwa baba na mama au wa kwa baba tu. Basi dada huyo atapata nusu ya mali yaliyoachwa na aliyefariki. Na iwapo aliyefariki ni huyo dada, na akawa hana mwana wala mzazi, basi kaka yake, wa kwa baba na mama au wa kwa baba, atarithi mali yote. Na iwapo yule aliyefariki, bila ya kuacha mwana wala mzazi, ana dada zake wawili, basi wao watapata theluthi mbili ya mali aliyoyaacha. Na watakapokusanyika pamoja kwenye urithi ndugu wa kiume na wa kike wasiokuwa wa kwa mama basi kila mmoja, katika ndugu wa kiume, atapata mfano wa mafungu mawili ya mwanamke. Mwenyezi Mungu Anawafafanulia namna ya kugawanya urithi na hukumu ya aliyefariki bila ya kuacha mwana wala mzazi, ili msije mkapotea kwenye njia ya haki kuhusu hukumu ya mambo ya uraihi. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzu wa mwisho wa mambo na yaliyo na heri kwa waja Wake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek